Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. Jenister Mhagama amezindua wiki ya Vijana Kitaifa akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasim Majaliwa Mkoani Manyara katika Viwanja vya Stendi ya Zamani na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Mwaka 2023 yanaenda sambamba na utunzaji wa Mazingira kufutia Tanzania kukumbwa na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi ambayo yameathiriwa na shughuli za wananchi. Hivyo Vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa Mazingira.Na kauli mbiu ya Mwaka huu ni “Vijana na Ujuzi rafiki wa Mazingira kwa maendeleo endelevu”.Pia Waziri Mhe. Jenister Mhagama amezindua kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Manyara na Dira ya Mkoa kwenye eneo la Uwekezaji na Maendeleo.
Vilevile amewashukuru timu nzima ya Mkoa wa Manyara kwa kazi nzuri na kubwa kwenye uzinduzi wa Jarida hilo. Ameongeza kuwa wameweka mazingira rafiki kwa kila atakayetaka kuwekeza ndani ya Mkoa wa Manyara na wameanza kutangaza fursa hizo kwa vijana waliofurika Mjini Babati kutoka pande zote za Tanzania katika wiki hii ya Vijana Kitaifa.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amesema wiki ya Vijana imeleta fursa kubwa kwa wananchi wa Manyara na Mkoa umekua kiuchumi hivyo anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa fursa hiyo Mkoani Manyara.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati