Na Nyeneu, P. R kwa kushirikiana na Afisa Habari wa OR-Utumishi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewasisitiza Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhakikisha kauli nzuri na huduma bora zinapewa kipaumbele kwa watumishi wa umma na wananchi wanaohudumiwa na ofisi yake. Mhe. Jenista ametoa maelekezo hayo Mjini Babati, wakati akifungua Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mhe. Waziri huyo amewataka watendaji wa ofisi yake kuwapokea vizuri na kutoa kauli nzuri kwa watumishi wa umma na wananchi pindi wanapowahudumia, kama ambavyo Mhe. Rais alivyowaamini na kuwapatia dhamana hiyo ya kuwahudumia kwa maslahi na maendeleo ya taifa. “Lugha nzuri wakati wa kumuhudumia mteja katika Ofisi ya Rais-UTUMISHI ni nyenzo muhimu katika utoaji wa huduma bora na haki kwa watumishi wa umma na wananchi wanaofuata huduma katika ofisi yetu, hivyo mnapaswa kuzingatia ili kufikia azma ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutoa huduma bora kwa kila mwananchi,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista amesema, Ofisi ya Rais-UTUMISHI ndio imepewa dhamana ya kusimamia maadili ya watumishi katika taasisi za umma, hivyo watendaji wa ofisi yake wanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kwa kuwa na maadili kiutendaji katika Utumishi wa Umma nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi hakusita kuwapongeza watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI kwa kufanya kazi kwa bidii maarifa katika kumsaidia Mhe. Jenista Mhagama na yeye mwenyewe kutekeleza jukumu walilopewa na Mhe. Rais la kumsaidia kusimamia vema Utumishi wa Umma ili uwe na tija katika kutoa huduma bora kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Cosmas Ngangaji kwa niaba ya wajumbe wa baraza na watumishi wote, amemshukuru Mhe. Jenista kwa kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati