Na Nyeneu, P. R
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imeanza rasmi kutumia mfumo wa kieletroniki wa kutoa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu. Halmashauri ya Mji wa Babati, imetenga fedha shilingi 155,741,173.70 ikiwa ni asilimia kumi (10%) kutoka kwenye makusanyo ya mapato ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.
Ili kuweza kuomba mikopo hii, waombaji wanatakiwa wawe na sifa zifuatazo; Kwanza kwa Vijana Wajasiriamali wawe na umri wa miaka 18 hadi 35, Wanawake wajasiriamali wawe na umri miaka 18 na kuendelea. Watu wenye ulemavu Wajasiriamali wa na umri kunzia miaka 18 na kuendelea. Waombaji wa mikopo wawe wakazi wa Halmashauri husika ambapo kwa Babati Mjini, wawe ni wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Waombaji wote wa mikopo wanapaswa kuwa raia wa Tanzania, pia wawe wamejiunga katika vikundi vya watu 5 - 30. Kwa muombaji mjasiriamali mwenye ulemavu asiye kwenye kikundi atapaswa awe na leseni ya biashara na hati ya utambulusho kutoka halmashauri ya Mji wa Babati. Watu wenye ulemavu wasio na leseni watajiunga kuanzia watatu na kujisajili kupitia mfumo na kupata hati ya utambulisho.
Aidha, vikundi vyote vinapaswa kuomba mkopo kwa kupitia mfumo wa maombi ya Mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia kiunganishi https://mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz, huu ni mfumo rasmi ambao umetengenezwa na kuratibiwa na OR – TAMISEMI. Pia waombaji wote wa mikopo wafike kwa Afisa Maendeleo ngazi ya Kata kwa maelezo zaidi.
Viambatisho vinavyohitajika
Faida za Mfumo
Aidha, Wananchi wote wa Halmashauri ya mji wa Babati wanahimizwa kutumia fursa hii ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi kwa kutuma maombi yao ndani ya muda wa siku 14 kuanzia tarehe 09/11/2022 na mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/11/2022 saa tisa na nusu alasiri (9:30).
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati