Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe.Pauline Gekul ameongoza kamati ya mfuko wa Jimbo kukagua miradi inayochangiwa na mfuko wa Jimbo .
Katika Ziara hiyo Mhe. Gekul amewaeleza Wananchi namna Serikali inavyowajibika kuwaletea Wananchi wake maendeleo kwa kusogeza huduma za afya, elimu na jamii karibu na Wananchi na kuwasaidia kupata maendeleo ya mtu mmoja mmoja, pia amewataka Wananchi kusimamia miradi hiyo kwa uaminifu Ili iweze kuwasaidia.
Kamati ya mfuko wa Jimbo imetenga zaidi ya Tsh. Millioni 63 kwa ajili ya kuchangia miradi ya maendeleo zikiwemo Zahanati, Shule, Ofisi za mitaa, pamoja na ujenzi wa Vyoo vya Wanafunzi.
Kwa upande wao Wananchi wamempongeza kwa Ziara hiyo na kueleza kuwa inasaidia kuongeza Uwajibikaji katika kuleta Maendeleo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati