Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Babati Bi.Anna Mbogo amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bw.Shaaban A. Mpendu ambapo, Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa kilomita 220.8 umezindua,umeweka mawe ya msingi na kutembelea miradi 8 yenye jumla ya shilingi Bilioni 4.92.
Katika mradi wa wanafunzi wenye mahitaji maalum Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw.Godfrey Eliakimu Mnzava amepongeza Walimu kwa kuendelea kuwatunza na kuwalea watoto hao na kuwapa elimu ya stadi za maisha kwa kuwafundisha kutunga shanga za urembo,kulima bustani ya mboga pamoja na stadi za maisha ya nyumbani ili ziweze kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.Pia ametoa wito kwa wazazi kutowafungia watoto wenye mahitaji maalum amewametaka kuwapeleka Shule ili kuweza kupata elimu kwani hakuna jambo linaloshindikana katika dunia ya sasa.
Aidha amesisitiza juu ya suala la kufanya manunuzi kwa kutumia Mfumo wa Kieletroniki wa Manunuzi ya Umma [Nest] na kuacha kufanya manunuzi katika miradi kwa kutumia njia ambayo Serikali imekataa ili kuweza kukamilisha miradi kwa ustadi na ufasaha kwa kuacha njia kutangaza zabuni katika mbao za matangazo kwa miradi yote.
Katika Banda la Ukatili wa kijinsia amewataka kitengo hicho kuendelea kufuatila matukio yote kwa ukaribu huku wakishirikiana na wananchi ii kuweza kupunguza na kutokemeza kabisa ukatili wa kijinsia na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kumalizana wenyewe.
Vilevile Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amsisitiza wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kuendelea kupanda miti katika mazingira yao ili kufanya mazingira kuwa mazuri na kutunza vyanzo vya maji kwa ujumla. Na kwenda sambamba na kuali mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 “ Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Sambamba na hilo Kiongozi wa Mbio za Mwenge ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kugombania nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa wale wenye sifa,kujiandikisha kwenye daftari la kudumu ili waweze kupiga kura kwa kumchagua kiongozi ambaye anafaa kuwaongoza kwa kushiriki katika mikutano ya kampeni itakapoanza.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati