Halmashauri ya Mji wa Babati imefanya mafunzo kwa kamati za mikopo ngazi ya Halmashauri,kamati za mikopo ngazi ya Kata pamoja na Timu ya menejimenti anbapo mafunzo hayo yamehudhuriwa na Watendaji wa Kata,Afisa maendeleo ya Jamii Kata,Afisa Ugani Kata,Mratibu wa Elimu Kata,Polisi Kata na Watendaji wa Mitaa na Vijiji katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Mafunzo hayo yanalengo ya kuwajengea uwezo wa namna ya utoaji na ufuatiliaji wa madeni ya mikopo isiyo na riba na Halmashauri ya Mji wa Babati imetenga jumla ya Milioni 626 ambazo zitatolewa hivi karibuni kwa makundi maalum( wanawake,vijana,na wenye ulemavu).
Aidha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw.Ally Mwinyikombo ameelezea majukumu ya Kamati hizo kuwa ni kupokea maombi ya mikopo,kuyajadili na kufanya tathimini kama maombi ya mkopo yamekidhi vigezo sambamba na kutembelea vikundi.
Pia Bw.Mwinyikombo amesisitiza kuwa wanufaika ni lazima wawe raia wa Tanzania,vikundi vyao vitambuliwe na Halmashauri na pia vikundi viwe na shughuli maalum ya kiuchumi inayoendelea.
Vilevile ameongeza kuwa kosa kisheria kwa Watumishi wa Serikali kupata mikopo hiyo au vikundi kuaandaa taarifa za uongo kwa lengo la kupata mikopo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati