Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yameendelea katika Shule ya Sekondari Aldersgate katika Jimbo la Babati Mjini Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi wameendelea kupata mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo zaidi katika ufanyaji wa kazi katika Kata,Vijiji na Mitaa watakazokwenda kufanya kazi.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo yameendelea vizuri na wanaimani na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayomertiki na Waandishi Wasaidizi wameelewa mafunzo na watakwenda kufanya kazi kwa weledi zaidi.
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Babati Bi Edna Moshi amefunga mafunzo rasmi amewataka kuwa na lugha nzuri,kuvaa mavazi ya heshima pia amesisitiza kufungua Vituo kwa wakati na wahakikishe mawakala wa Vyama vya Siasa kutokuingilia Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Vituo vyao.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati