Wizara ya Elimu Sayansi naTeknolojia kupitia Taasisi ya Elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati imetoa mafunzo kwa Walimu wa Shule ya Awali na Msingi zilizopo katika Kata zote 8 Halmashauri ya Mji wa Babati.
Mafunzo maalum kwa Walimu wa Shule za Msingi kuhusu Mtaala ulioboreshwa yamefanyika katika Vituo 3 vinavyojumuisha Kata zote 8 zilizopo Halmashauri ya Mji Babati.Ambapo Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Aldersgate,Shule ya Sekondari Kwaraa pamoja na Kituo cha Walimu Managha.
Wakufunzi katika Mafunzo hayo ni Maafisa Elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Babati,Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule Halmashauri ya Mji Bi.Elizabeth Isaya Tarmo,Wathibiti Ubora wa Shule na Maafisa Elimu Kata zote 8 pamoja na Walimu wa Awali waliopata mafunzo ngazi ya Taifa.
Mafunzo hayo yanalengo ya kuwafikia Walimu takribani 628 kwa Shule za Msingi za Serikali na zisizo za Serikali.Miongoni mwa mada zinazotelewa ni sababu za mabadiliko katika Mtaala wa Elimu Muundo mpya wa Elimu,Matumizi ya Tehama,Maandalizi ya nyaraka za ujifunzaji na ufundishaji,Maandalizi ya zana za ujifunzaji na ufundishwaji,Upimaji na Tathmini pamoja na Ushauri na Unasihi.
Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Simon Mumbee amewapongeza Walimu kwa kazi zuri wanazofanya katika kuwafundisha Wanafunzi na kupata matokeo mazuri amewataka kuendelea kufundisha kwa weledi zaidi na ili kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi wa madarasa yote ya Shule ya Msingi pamoja na kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa na Wakufunzi ili wakayatumie vizuri.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati