Mkoa wa Manyara umeadhimisha Siku ya Wanawake 8/03/2024 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo Viongozi mbalimbali wameudhuria na mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga.
Mhe.Sendiga amesisitiza suala la kushirikiana ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii wanawake jeshi kubwa jambo hili lazima litokomezwe ili kuwepo na jamii yenye tija na ni jukumu la kila mtu kufichua vitendo hivyo na sio kuvifumbia macho havistahili katika jamii. Na Sheria lazima ifuate mkondo wake kwa yeyote atakayefanya vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa wengine.
Pia ameongeza kuwa lishe ni muhimu ili watoto wawe na afya njema katika jamii na kusaidia watoto kukua vizuri kwa ujumla Halmashauri ya Mji wa Babati imetenga Bilioni 1 kwa ajili ya lishe.
Aidha Mhe.Queen amesema kuwa wanawake wajifunze kupitia majukwaa ambayo yameendelea kuwepo ili kuweza kuwa na mabadiliko katika jamii katika sekta ya uchumi na nyinginezo pia ameongeza kuwa wanawake wametakiwa kusaidiana na kushirikiana.Ili kuenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu Wekeza kwa Mwanamke kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii.
Vilevile Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Sendiga amesisitiza juu ya suala la usafi wa mazingira hasa wakati huu wa magonjwa ya mlipuko ni muhimu sana kwa kutumia vyoo safi na salama na kuweka mazingira katika hali ya usafi wakati wote.
Sambamba na hilo Mhe. Sendiga ametembelea banda la TRA,RUWASA,BAWASA na TANESCO pamoja na mjasiriamali aliyekuwepo uwanjani hapo pia amewataka wanawake kuendelea na jukumu la kulea watoto katika maadili mazuri na amewasisitiza kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati