Afisa Lishe wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi Namsifu Godson akizungumza na watendaji wa mitaa na wahudumu wa Afya kwenye Kata za Bagara,Bonga, singe, Sigino zilizopo Halmashauri ya Mji wa Babati,
Lengo ni:-
i. Kuelimisha watendaji wa kata, vijiji na mitaa katika kusimamia utekelezaji wa ukusanyaji wa takwimu wa viashiria vya lishe vilivyopo katika mkataba wa lishe ngazi ya kata/vijiji/ mitaa.
ii.Ufafanuzi ulitolewa katika kuhakikisha kuwa watoto wote chini ya miaka 5 wanapimw hali ya lishe na kuhakikisha taarifa hizo zinabandikwa katika mbao za matangazo za kata ,vijiji na mitaa.
iii.Kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa maadhimisho ya siku na afya na lishe ya kijiji/mitaa kila baada ya miezi mitatu
iv.Ufafanuzi juu ya kuchukua idadi ya wanaume walioshiriki katika siku hii na kupata elimu ya lishe ili kwa pamoja wanafamilia wazingatie lishe bora katika ukuaji bora na afya bora kwa mtoto wao
v.Wahudumu ngazi ya jamii kuwasilisha taarifa/takwimu kwa watendaji wa vijiji/mitaa kwa wakati ili zifikie ngazi ya kata na Halmashaur kwa wakati waliokubaliana
vi.Wahudumu wa afya ngazi ya jamii kutoa rufaa kwa wakati kwa watoto ambao wamegundulika na utapiamlo mkali kwenda kituo cha afya kilichopo karibu
Ziara hii imekuja baada ya kikao cha tathmini ya takwimu hizi kwa robo iliyopita na kuonekana kuwa maeneo hayo hayakuripotiwa vizuri , Hii itapelekea kuwa na taarifa na takwimu bora katika kufanya maamuzi kama Halmashaur, Mkoa na Taifa kwa ujumla
Akiwa kata ya Bagara Akiwa kata ya Sigino
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati