Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Cuthbert Sendiga amewaongoza wananchi wa Arusha, Manyara na Kilimanjaro kwenye kilele cha maadhimisho ya nanenane yaliyofanyika kanda ya kaskazini Themi-Njiro jijini Arusha.
Mhe. Queen Sendiga akiwa mgeni rasmi wa tukio hilo kubwa ametembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho pamoja na kuhutubia Umma uliojitokeza amewataka kutumia fursa iliyopo katika kilimo ili kukabiliana na mabadililko ya tabia ya nchi.
Pia Mkuu wa Mkoa wa Manyara ametoa rai kwa Wataalamu na Maafisa wa kilimo kuyafikia makundi ya wanawake, vijana na wananchi kwa ujumla ili kuwaongezea elimu na ufanisi katika shughuli za kilimo na ufugaji ili kujipatia tija.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ameridhishwa na maandalizi yaliyofanywa na halmashauri hizo pamoja na elimu inayoendelea kutolewa na wananchi katika sekta ya kilimo,uvuvi na ufugaji.
Vilevile kanda ya kaskazini Halmashauri ya Mji wa Babati imepata mshindi katika sekta ya kilimo na ufugaji Bw. John Laizer na katika mabanda Halmashauri imeshika nafasi ya pili ambapo ni mifugo na kilimo.
Aidha amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya umwagiliaji kwenye ukanda wa Mikoa ya kaskazini yenye thamani ya Bilioni 47.64. Vilevile ameeleza mpango wa Serikali katika ujenzi wa visima 150 kwa kila Halmashauri ili kuleta mapinduzi katika Sekta ya Umwagiliaji.
Pia Mhe. Queen Sendiga ameongeza siku mbili zaidi kwa maonyesho hayo kuendelea katika viwanja hivyo baada ya kuridhishwa na maonyesho kwa wakulima, wananchi na wanafunzi waliyojitokeza kujifunza kupitia maonyesho hayo. Amewataka wataalamu na maafisa wasichoke kutoa elimu katika maonyesho hayo.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati