Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi. Karoline Mthapula amefanya kikao Maalum cha Mafunzo ya Maadili kwa Utumishi wa Umma Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo kimeudhuriwa na Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali Watu Bw.Dominic Mbwette,Katibu Tawala Wilaya,Bw.Simon Mumbee kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati ,Viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara pamoja na Watumishi wote katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati.
Bi. Karoline amesisitiza maadili mazuri kwa Mtumishi wa Umma muda wote anapokuwa kazini na nje ya kituo cha kazi na kutoa huduma bora kwa wateja pamoja na kuzingatia suala la mavazi. Maadili mazuri huchochea utoaji wa huduma bora zaidi.
Pia Bw.Dominic Mbwette ambaye amewataka Watumishi wa Umma kutii sheria bila shuruti na kuwa mfano kwa wananchi wengine kwa kufuata Sheria, Taratibu na Miongozo yote ambayo Mtumishi wa Umma ametakiwa kufuata kwa ujumla. Pamoja na hilo amesisitiza kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa zaidi.
Aidha Bw. Mbwette ameongeza kuwa Mtumishi wa Umma ametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kutunza siri za Serikali kwa kuzingatia Miongozo na Sheria.Pia kutumia barua pepe za SerikaIi kwa matumizi ya Kiofisi tu na sio vinginevyo na kusisitiza kuwa Mtumishi ametakiwa kutotumia mitandao ya Kijamii wakati wa kazi.
Vilevile Bw. Mbwette amewataka Watumishi wa Umma kutumia Mifumo ya Kieletroniki ambayo Serikali imeleta ili kupunguza matumizi ya majalada na kuongeza ufanisi zaidi katika utendaji wa kazi kiujumla ndani ya Halmashauri zote Nchini na amesisitiza matumizi ya Mfumo wa e mrejesho ambao unatoa fursa kwa Mtumishi wa Umma pamoja na wananchi kutoa maoni,mapendekezo,malalamiko na pongezi.
Sambamba na hilo Bi.Karoline Mthapula ameongeza kuwa miradi ya maendeleo imetakiwa kusimamiwa kwa umakini, kusikiliza kero za wananchi ni muhimu sana pamoja na kuzitatua zile zilizopo ndani ya ngazi ya Halmashauri,kuendelea kupinga ukatili wa Kijinsia na amesisitiza sana juu ya ubunifu wa vyanzo vingine vingi vya mapato ambavyo vitaongezea mapato na kufanya Halmashauri kuzidi kujiimalisha katika ukusanyaji wa mapato.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati