Kampuni ya Carbon Tanzania imewakabidhi mfano wa hundi ya Billioni 4.7 ikiwa ni malipo ya uuzaji wa hewa ya ukaa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Sulemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga pamoja na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul katika Ukumbi wa WhiteRose Mkoani Manyara kwa Utunzaji wa Mazingira.
Mhe.Jafo ameipongeza Kampuni ya Carbon kwa kufanya biashara ya hewa ya ukaa imesaidia katika suala zima la utunzaji wa mazingira na ni fursa kubwa ambayo imewawezesha kupata mapato nje ya vyanzo vingine.Na amesema kuwa Wizara imekuja na miongozo na kanuni za biashara ya hewa ya ukaa katika Taifa letu, kupitia fedha hewa ya ukaa imesaidia katika Ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa takribani makampuni 53 yameanza kufanya biashara ya hewa ya ukaa.Vilevile ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuwa wawazi katika biashara hususani suala la mapato hiyo ni hatua nzuri katika ukuaji wa kibiashara kwa ujumla.Mhe.Jafo amewataka wananchi kutunza misitu, misitu ni mali inapaswa kulindwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga ameishukuru Kampuni ya Carbon Tanzania kwa hundi ambayo imewapatia na kwa kazi nzuri ya utunzaji wa mazingira,wananchi wamepata Elimu juu ya faida ya utunzaji wa misitu. Na ameongeza kuwa takribani wananchi 64,000/=wamenufaika na mradi huo wa hewa ya ukaa. Baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kiteto na Wilaya ya Mbulu wameanza kunufaika na mradi wa hewa ya ukaa tangu mwaka 2017.
Mkurugenzi wa Carbon Tanzania Bw.Alphan Jackson amesema kuwa kutunza vyanzo vya maji, kulinda misitu ni jukumu la kila mmoja wetu kulinda na hii imesaidia sana katika biashara ya hewa ya ukaa. Ameishukuru Serikali kwa kuweka mfumo rahisi na wezeshi katika shughuli za biashara ya hewa ya ukaa.
Sambamba na hilo ametembelea Ziwa Babati na kuona na namna Vijana wanavyosafisha Ziwa kwa kuondoa magugu ameahidi kufuatilia ili kuapata njia nzuri zaidi ya kuondoa magugu hayo ndani ya Ziwa na kulete muonekano mzuri wa Ziwa kwa ujumla.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati