Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI[Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa] ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Dennis Lazaro Londo pamoja na Wajumbe wa kamati imetembelea mradi wa Barabara ya TARURA[Wakala ya Barabara za Mijini na Vijijini] Kona ya Nakwa pamoja na mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Manyara katika Kijiji cha Kiongozi,Kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati.
Halmashauri ya Mji wa Babati ilipokea jumla ya Shilingi 3,000,000,000.00 kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari [SEQUIP] kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkoani Manyara.Ambapo mpaka sasa kuna majengo ya mabweni 8,Nyumba 2,Bwalo 1,Jengo la Utawala 1,Jengo la Wagonjwa 1,Madarasa 12,Maabara 4,Chumba cha Jenereta 1 pamoja na Choo chenye matundu 16.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge TAMISEMI imetoa pongezi nyingi sana kwa usimamizi mzuri wa mradi hadi kufikia hatua hiyo ushirikiana na umoja uendelee ili mradi uweze kukamilika kwa wakati na Mhisani Ndugu Baba Atia aliyejitolea kuchimba kisima ili kuwezesha upatikanaji na maji katika ujenzi huo mchango wake utambulike kwa ngazi zote kuanzia Mkoa mpaka Kijiji ili iwe chachu kwa wengine kuweza kujifunza.
Vilevile Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi ameongeza kuwa suala la mabafu ni changamoto kwa idadi ni machache Wanafunzi watatumia muda wingi kujindaa kwenda Shule imetakiwa kuangalia namna ya kuongeza ili ipunguze muda wa maandalizi ya asubuhi kwa Wanafunzi Shuleni.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Dennis Londo ametoa pongezi nyingi kwa mafundi ni wazuri na wataalam sana majengo hayana kasoro na amepata uzoefu juu ya Force Account kuwa ni nzuri endapo itasimamiwa kwa umakini.Pia amepongeza kuwa ushirikiano uliopo na Taasisi nyingine inapendeza sana kushirikiana ili kufanikisha ujenzi na kwenda kwa haraka chini ya Kiongozi mahiri Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga pamoja na Viongozi wengine wote.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati