Jimbo la Babati Mjini laendesha mafunzo ya Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata
Imechapishwa: August 7th, 2020
Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha taratibu mbalimbali za Kikatiba, Kisheria, Kikanuni pamoja na maelekezo ya Tume ambazo watendaji wa uchaguzi wanapaswa kuzingatia. Jimbo la Babati Mjini laendesha mafunzo kwa Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata leo Tarehe 7 Mwezi Agosti 2020 kwa kadri ya maelekezo ya Tume ya Uchaguzi. Mafunzo hayo ambayo yameanza leo yatachukua siku tatu yaani kutoka tarehe 7 hadi 9 Mwezi Agosti 2020. Katika mafunzo hayo, wanasemina (wasimamizi wasaidizi) wameaswa kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na kwa weledi.
Kushindwa kuzingatia taratibu za uchaguzi kunaweza kuwa na athari katika zoezi zima la uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuharibu imani ya wadau wa uchaguzi na kusababisha malalamiko ya kutoridhishwa na mchakato.