• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Halmashauri zahimizwa kuendelea kupanda miti ili kufikia lengo la Mwaka la Mkoa

Imechapishwa: April 25th, 2023

Na Nyeneu, P. R - Dongobesh

Kufuatia maelekezo ya serikali kuwa maadhimisho ya sherehe za Miaka 59 ya Muungano kwa mwaka huu zifanyike katika ngazi ya Mikoa nchini kote, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere leo tarehe 25 Aprili, 2023 ameungana na viongozi mbalimbali wa Mkoa akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa na wananchi wa Wilaya ya Mbulu kushiriki zoezi la Upandaji miti 154 kwenye eneo la Hospitali ya Wilaya ya Mbulu na eneo la jengo la utawala la Halmashauri Mjini Dongobesh miti 258 hivyo kufanya jumla ya miti 412.

Lengo la kuadhimisha maadhimisho katika ngazi ya mikoa ni kuwapa fursa wananchi kuelewa kwa undani maana ya Muungano ulioasisiwa na waasisi wetu. Katika Hafla hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema amefarijika sana na Muitikio wa wananchi wa eneo hilo kushiriki zoezi la upandaji miti. “Binafsi nimefarijika sana kuona muitikio wenu katika shughuli hii muhimu kwa ustawi wa nchi yetu na Maisha yetu”. Alisema Mhe. Makongoro.

Aidha, katika taarifa yake Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri Bi. Pellagia Shirima amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ilianza kujengwa mwezi Machi, 2019 baada ya kupata fedha za ujenzi kutoka Serikali Kuu. Katika Kipindi cha mwaka 2018/2019 hadi 2022/2023 Halmashauri ilipokea fedha Shilingi Bilioni 2.76 kwaajili ya ujenzi wa majengo ya Hospitali ambapo shilingi Bilioni 2.69 ni kutoka serikali kuu na shilingi Milioni 70 ni fedha za Mapato ya ndani. Mapokezi ya fedha hizi yamewezesha kujengwa kwa majengo 12 ikiwemo nyumba ya mtumishi ya 3 in 1 na Hospitali ilishaanza kutoa huduma tangu tarehe 03 Aprili, 2023

RC Makongoro ametoa wito kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha miti yote iliyopandwa katika eneo la Hospitali inatunzwa vizuri na pia amesisitiza uhamasishaji wa upandaji miti katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara unaendelea ili kufikia lengo la upandaji miti 1,500,000 kwa mwaka kwa Mkoa mzima.

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati