Halmshauri ya Mji wa Babati imepanga kutumia jumla shilingi bilioni Ishirini na tatu milioni mia nne thelathini na tano laki tatu thelathini na saba elfu mia tano arobaini na saba (Tshs 23,435,337,547) ikiwa shilingi 17,319,294,000/= kwa ajili ya mishahara, shilingi 705,150,050/= Matumizi ya kawaida, shilingi 3,510,306,047 ruzuku ya Miradi ya Maendeleo na shilingi 1,900,587,450 kutoka vyanzo vya ndani vya Halmashauri kwa ajili ya bajeti ya Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Akiwasilisha mapitio ya bajeti ya mwaka 2018/2019 katika mkutano maalum wa Baraza la Mdiwani uliofanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mchumi wa Halmashauri Bwana Khamis Katimba alisema kuwa maeneo yatakayopewa kipaumbele kwa ajili ya utekelezaji huo ni Kuendelea kukamilisha miradi ambayo haijakamilika katika sekta mbalimbali, Kulipa madeni ya wakandarasi na madeni mengine, Kuendelea kujumuisha masuala mtambuka katika mpango wa bajeti (UKIMWI, Mazingira na Jinsia), Kuongeza maeneo ya Vitega uchumumi kama Stendi mpya, kuboresha masoko na Biashara comlex maarufu kama Motel Papaa) kwa njia ya PPP pamoja na Kuwajengea uwezo Waheshimiwa Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Mji.
Aidha, Mchumi wa Halmashauri ya Mji wa Babati akitoa mwelekeo wa mpango na Bajeti hiyo alilimbia Baraza la Madiwani kuwa Halmashauri itajitahidi kuingia ubia na wadau mbalimbali katika uwekezaji wa miradi itakayokuwa vyanzo vya kudumu vya mapato kwani uwekezaji utakuwa na tija kubwa kwa kutokakana na fursa za uwekezaji kama Viwanja vilivyopimwa katika Eneo la Maisaka Katani, Shamba la Hanadeco, hali nzuri ya hewa na Mji kuwa kwenye Barabara kuu ya Afrika Kusini hadi Cape Town (The Great North Road or Pan – Africa Highway), pia kutokana na Mji wa Babati kuwa karibu na Makao makuu ya Nchi Dodoma, Uwepo wa Mlima Kwaraa ambao ni kivutio kwa watalii wa ndani na nje ya nchi kuupanda na uwepo wa ziwa Babati lenye viboko wapole hizo zote ni fursa zilizopo katika mji wa Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati