Halmashauri ya Mji wa Babati imekabidhi vitambulisho kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo 158 wakiwemo Machinga, Madereva wa Pikipiki,Bajaji mama lishe na Baba lishe. Katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Babati.
Vitambulisho hivyo Vimeandaliwa na Kituo cha Taifa cha kuhifadhi data kimtandao (NIDC) Kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii na OR-TAMISEMI kwa lengo la kuwainua kiuchumi wafanyabiashara wadogo wadogo.
Akikabidhi vitambulisho hivyo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Mwinyikombo ameeleza kuwa Vitambulisho hivyo vina umuhimu mkubwa sana kwa wajasiriamali kwakuwa itawasaidia kutambulika na Mamlaka mbali mbali za kiserikali, kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha, kuunganishwa na mifuko ya jamii, Pamoja na kulipia huduma mbalimbali katika vituo vya kutolea huduma Nchini.
Vile vile ametoa ufafanuzi kuwa vitambulisho hivyo vinatolewa baada ya Mfanyabiashara kukamilisha taratibu zote za usajili katika Mfumo, kulipa kiasi cha shilingi 20,000/= kupitia nambari ya udhibiti (control number). Pamoja na hilo ameeleza kuwa vitambulisho vitadumu kwa muda wa miaka mitatu mfanyabiashara atatakiwa kuhuisha tena kitambulisho chake baada ya kuisha muda wa Matumizi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati