Halmashauri ya Mji wa Babati imeagizwa kuanza mchakato wa kujenga Ofisi za Kata,Mitaa na Vijiji ili kuipunguzia Halmashauri gharama za uendeshaji wa ofisi.
Hayo yamesemwa jana (Jumatatu) 5/2/2018 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mh. Kibiki M.Kibiki wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mheshiwa Kibiki aliwataka wataalam wa Halmashauri hiyo kutafuta maeneo hayo kwa kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika ili wananchi hao watoe maeneo ya kujenga ofisi hizo na kupewa fidia.
Mwenyekiti alisisitiza kuwa ujengaji wa ofisi hizo utaisaidia Halmashauri kupunguza gharama za uendeshaji wa Ofisi ambazo zinatumia gharama kubwa saba kulipia pango ili pesa zitakazookolewa zitumike kwa shughuli nyingine kwa maendeleo ya wananchi.
Mpaka sasa Halmashauri ina Ofisi za Kata tano kati ya nane, ofisi za mitaa mbili kati ya thelathini na tano na Ofisi za Vijiji mbili kati ya Vijiji kumi na tatu.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati