Halmashauri ya Mji wa Babati imemaliza zoezi la kupiga chapa ng’ombe wote wa asili kwa kata zote 8.Zoezi lililoanza mwezi Oktoba hadi Desemba 2017 baada ya kupata agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitolewa mwezi Desemba 2016 .
Katika zoezi hilo, Halmashauri ilikuwa na lengo la kupiga chapa ng’ombe 21,619 ambapo baada ya zoezi la upigaji, jumla ya ng’ombe 27,110 walipigwa chapa ambayo ni sawa na asilimia 125.4 ya lengo walipigwa chapa.
Akiongea na Mwandishi wa habari hii Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Mji wa Babati BI. Rena Urio alisema Zoezi la kupiga chapa ng’ombe wa asili limekamilika na sasa wanasubiri maelekezo ya upigaji wa chapa kwa ng’ombe wa kisasa.
Zoezi hilo limechelewa kuanza mapema kutokana na kutakiwa kupitishwa kwenye vikao mbali mbali vya Halmashauri ambavyo vipo kisheria.
Aidha Baraza la madiwani kwa pamoja liliridhia gharama ya Tsh. 500 kwa kila ng’ombe atakayepigwa chapa kama ilivyotolewa kwenye maelekezo ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na wataalam wa mifugo nchi nzima Mjini Dodoma.
Pia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ilitoa namba za utambulisho wa chapa kitaifa na ngazi ya Halmashauri ambapo Halmashauri ya Mji wa Babati ilipewa namba T – BAT. T – inawakilisha Tanzania na BAT – inawakilisha Babati Town. Hata hivyo baada ya utambulisho huo Halmashauri ilipewa mamlaka ya kutoa namba kwa kila kijiji.
Faida ya zoezi hili ni kama ifuatavyo:-
Hasara za kutokupiga chapa
Kutokufanya zoezi hili ni kupinga agizo la Mh. Makamu wa Rais hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.
Baada ya upigaji chapa hakuna ng’ombe yeyote atakaye uzwa au kununuliwa ndani na nje ya Halmashauri bila kuwa na namba ya usajili.
Ng’ombe atakayekamatwa bila chapa atatambuliwa kuwa ni wa wizi.
IDADI YA NG’OMBE WALIOPIGWA CHAPA KILA KATA .
NA
|
KATA
|
LENGO NG’OMBE
|
HALI HALISI NG’OMBE
|
ASILIMIA(%)
|
1
|
BABATI
|
1050
|
1086 |
103.4 |
2
|
BAGARA
|
3750
|
4245 |
113.2 |
3
|
BONGA
|
2215
|
2428 |
109.6 |
4
|
MAISAKA
|
3627
|
5422 |
149.5 |
5
|
MUTUKA
|
3027
|
5257 |
173.7 |
6
|
NANGARA
|
1660
|
1665 |
100.3 |
7
|
SIGINO
|
4620
|
5037 |
109.0 |
8
|
SINGE
|
1670
|
1970 |
118.0 |
|
JUMLA KUU
|
21619
|
27110 |
125.4 |
|
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati