Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuella Kaganda, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, CPA Shaaban A.Mpendu, kwa kukusanya Mapato na kusimamia vyema mchakato wa utoaji wa mikopo ya 10% hasa kwa vijana wanao jihusisha na Shughuli za usafirishaji ,na kusema kuwa itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana
Mkuu wa Wilaya ya Babati Kaganda amekabidhi mfano wa Hundi yenye jumla ya TZS Mil.211.216 ya awamu ya kwanza katika ukumbi wa Halmashauri, ambapo Milioni 161 zimetolewa kwa vijana na Milioni 50 kwa wanawake.Mhe.Kaganda amesisitiza wanufaika kutumia vyema mikopo hiyo ili iwe na tija kwenye Maisha yao na kuchangia katika Maendeleo ya jamii. Pia amewataka kuwa wazalendo, kuepuka tabia za ushawishi vibaya badala yake kujiwekea sheria zitakazo waongoza katika Shughuli zao.
Akisoma Risala kwa niaba ya wanufaika wote Bw. Almas Said amesema kuwa‘Tunampongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kutupatia mikopo hii kwa Haki bila ubaguzi,nasi tunaahidi tutakuwa waaminifu katika kurejesha na pia tunamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuirejesha mikopo hii’
Sambamba na hilo Mhe. Kaganda amekabidhi Spika nane kwa Maafisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata kwa kata zote nane za Halmashauri ya Mji wa Babati Spika zitakazotumika kwa Shughuli mbali mbali za Serikali yakiwa ni maelekezo ya Waziri wa Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati