• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Hali ya Mradi wa Vibanda vya Biashara uwanja wa Kwaraa

Imechapishwa: September 17th, 2020

Imeandikwa na Nyeneu, P. R

Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Babati pamoja na kikosi kazi leo tarehe 17 septemba 2020 ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mji Bw. Luther Daniel wametembelea mradi wa vibanda vya biashara unaoendelea katika uwanja wa michezo wa Kwaraa, kufanya ukaguzi na kubaini vibanda vilivyoendelezwa kujengwa na ambavyo bado wadau wa vibanda hivyo wanasuasua kuviendeleza.

(Picha: Nyeneu, P. R) Mchumi Bw. Godlisten Geoffrey (Kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Menejimenti kuhusu mchakato mzima wa ujenzi wa vibanda vya Biashara uwanja wa Kwaraa.


Timu ya Menejimenti imefanya ukaguzi huo kufuatia tangazo la tarehe 15 Agosti 2020 la kuwataka wadau ambao hawajaendeleza ujenzi hadi kufikia tarehe 30 Agosti 2020 wanyang’anywe eneo na azimio hilo linaendelea kutekelezwa kwa wale wote ambao hawajaendeleza ujenzi katika maeneo hayo. 

Hadi kufikia tarehe 16 Septemba 2020, idadi ya maeneo ya ujenzi wa vibanda 136 tayari wamepatiwa wadau mbalimbali ili kuendeleza ujenzi, ambapo ujenzi huo umefikia katika hatua nzuri kwani vibanda 07 vipo hatua ya kenchi, vibanda 08 vipo katika hatua ya lenta ya juu, Vibanda 13 vipo hatua ya Jamvi (Hatua ya kwanza ya ujenzi umekamilika), Vibanda 79 vimejengwa msingi, kuwekwa Kifusi na kupangwa mawe. Aidha Vibanda 10 vimewekwa zege la awali (Blinding) na Maeneo 19 ya ujenzi wa vibanda havijaendelezwa ujenzi bali vimechimbwa msingi tu. Pia ni wadau 20 tu ndo waliojitokeza kujaza mikataba ya ujenzi kati ya wadau 136 waliopewa maeneo.

(Picha: Nyeneu, P. R). Baadhi ya vibanda ambavyo ujenzi umefikia katika hatua ya Kenchi kama inavyoonekana katika picha.


Aidha, hadi kufikia sasa mradi umekuwa na mafanikio mbalimbali kwa wanajamii kwani ujenzi bado unaendelea na wadau wameitikia kwa viwango na mradi umepokelewa kwa mtazamo chanya kwa wananchi wa Mji wa Babati. Pia mradi huu umewanufaisha wananchi wa eneo hilo kuanzia wauzaji wa material na vifaa mbalimbali vya ujenzi, madereva wa malori, na pia kutoa ajira kwa vijana nguvu kazi katika ujenzi. Kukamilika kwa mradi huu kutabadilisha muonekano wa Mji wa Babati na uwanja huo wa michezo kwa ujumla.


Ujenzi wa Vibanda katika hatua ya Lenta ya juu
Ujenzi wa Vibanda katika hatua ya jamvi


Pamoja na kuwepo na mafanikio mbalimbali katika kutekeleza mradi huu, kumekuwepo na changamoto kadhaa kama vile wadau kubadilishana vibanda wenyewe kwa wenyewe bila kumfahamisha Mkurugenzi wa Mji, Pia Changamoto nyingine ni wadau kutapeliana, wizi wa vifaa vya ujenzi(Material) pamoja na fedha. Pia ujenzi unaendelea kwa kusuasua – (kasi ya ujenzi kuwa ndogo) ambapo matarajio ya mradi ni kwamba hadi ifikapo tarehe 30 Desemba 2020 mradi unapaswa kukamilika.- Alieleza mchumi.

(Picha: Nyeneu, P. R) Moja kati ya maeneo ya vibanda ambayo hayajaendelezwa. Ujenzi wake umeishia katika hatua ya kuchimba msingi tu

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati