Project manager wa Miradi inayofadhiliwa na Norwegian Church Aid (NCA) kupitia ELCT -Northern Diocese Rev. Andrew Munisi (watatu kushoto- mwenye Tshirt), Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Bwn Daniel Luther(kulia kwake)katika picha ya pamoja na viongozi wa PETS (Public Expenditure Trucking System), Paralegals, viongozi wa VICOBA, kamati za mawasiliano ya dini mbalimbali (Interfaith) wataalamu wa kilimo na maendeleo ya jamii katika kikao kilichofanyika tarehe 19/8/2019 kwenye ukumbi wa Whiterose Babati Mjini.
wananchi wa kata zote za Mji wa Babati ni wanufaika wa huduma za kitaalamu na fedha katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji, ufugaji wa kuku walioboreshwa, ujenzi wa madarasa, ofisi za vijiji, zahanati nk.