Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi. Pendo Mangali amezindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto( PJT-MMMAM)ngazi ya Halmashauri katika Ukumbi wa Mji.Ambapo uzinduzi huo ulihudhuriwa na Madiwani,Wakuu wa idara,Watumishi wa Halmashauri waandishi wa habari na shirika la COSITA.
Bi Pendo Mangali ameshukuru kwa (PJT-MMMAM) kuzinduliwa ndani ya Halmashauri na amewataka watumishi wote kuhudhuria ili kupata elimu juu ya malezi ya watoto ambao umri wao ni kuanzia mwaka 0-8 kwa mujibu wa program hii. Ili tukawe mabalozi kwa wananchi wengine kwa kuwapa elimu juu ya utekelezaji wa (MMMAM) katika jamii zetu.
Pia Bi. Khadija Muwango Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa amesema kuwa watoto ili wakue vizuri kimwili,kiakili,kihisia,kimaadili, afya na lishe lazima yawe sawa.Na wazazi ni wajibu kulisimamia hilo kwa namna moja au nyingine katika jamii ili tupate kizazi chenye maadili kwa miaka ijayo.
Aidha ameongeza kuwa ulinzi na usalama wa mtoto ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha hilo linatokea na kuacha kuficha vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa Watoto kwa kuripoti matukio hayo itasaidia kutokomeza kwa hatua kali zitakazochukuliwa dhidi ya watakaobainika kuwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo.
Vilevile amesema Afya bora, Ulinzi na Usalama,Elimu ya Awali,Lishe bora na Malezi yenye uwitikio ni muongozo wa ukuaji timilifu wa mtoto hivyo wazazi wanatakiwa kuzifuata na kuzitekeleza kwa maslahi mapana ya ukuaji mzuri kwa mtoto.
Bw. Agustino Balohho Afisa mradi wa “Mtoto Kwanza” Shirika la COSITA amesisitiza kuwa wazazi wametakiwa kujenga ubongo wa mtoto tangu akiwa mtoto na anapofikisha umri wa miaka 6 anakuwa na asilimia 100 ya ubongo wa mtu mzima,mtoto anajifunza na kujenga ushirikiano wakati anapokuwa anacheza na unaweza kutambua kipaji cha mtoto wakati huo.
Pia ameongeza kuwa Watoto wametakiwa kupata lishe na mazingira wezeshi ya kujifunza kwa kuwajengea madarasa yanayozungumza ili kuwasaidia kujifunza kwa wepesi na haraka zaidi pamoja na kuwawezesha walezi wa Watoto katika shule za awali.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati