Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman H. Kololi ameliongoza Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo Baraza hilo limeudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali,Madiwani wa Kata zote,Wataalam,Viongozi wa Taasisi,Katibu wa Chama cha Mapinduzi Halmashauri ya Mji pamoja na waalikwa wengine.
Katika Baraza hilo la Madiwani limepitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti ya Mwaka 2024/2025 ambapo Jumla ya Shilingi 29,329,213,000.16 imepitishwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kawaida na maendeleo kwa kipindi cha Julai hadi Juni 2024/2025.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali amesema kuwa Bajeti hiyo imefuata mwongozo wa Serikali wa uandaaji mpango wa Bajeti umezingatia vipaumbele vya Halmashauri pamoja na vya Nchi kwa ujumla.Ameongeza kuwa Halmashauri ya Mji wa Babati itakamilisha miradi ambayo imepangwa na bajeti hiyo pamoja na kuitetea katika ngazi ya Mkoa na hatimaye Bungeni.
Aidha Ndugu Mohamed Cholage amewapongeza Wataalam,Madiwani pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kazi nzuri ya uandaaji wa mpango wa Bajeti wa Mwaka 2024/2025 katika Halmashauri pamoja na kuzingatia vipaumbele na amesisitiza juu ya utekelezaji wa Bajeti hiyo kupanga ni kitu kingine nautekelezaji ni jambo lengine hivyo amehimiza utekelezaji wa Mpango huo wa Bajeti.
Pia Mhe.Kololi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za miradi zinazoletwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Kata zote 8 zilizopo ndani ya Halmashauri ya Mji amesisitiza kuwa miradi yote itakamilika kwa wakati.
Sambamba na hilo Bi.Pendo Mangali amesema kuwa bajeti hiyo ambayo imepitishwa itatekelezwa kwa vitendo na umakini mkubwa mno pamoja na kukamilisha miradi yote ambayo ni vipaumbele kwa kila Kata na miradi mingine yote ambayo ipo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Babati kwa ujumla.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati