Jumla ya Wanufaika 1621 wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Halmashauri ya Mji wa Babati wamepokea malipo ya pesa ya kuwainua kiuchumi ya dirisha la mwezi Septemba na Oktoba tarehe 30 na 31 Desemba 2024.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Babati Bi. Edna Moshi ameeleza kuwa jumla ya Tsh. 50,560,000/= zimelipwa kupitia mitandao ya Simu, akaunti za benki za wanufaika na baadhi wamepokea fedha mkononi.
Pia ameeleza kuwa mkakati uliopo ni kuhakikisha malipo yote yanafanyika kwa njia ya mtandao na Benki.
Pamoja na hilo Wanufaika wamepewa elimu juu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia ikiwa ni mkakati wa Taifa Ili kuwasaidia Wanufaika kuepuka athari zinazotokana na matumizi ya Nishati isiyosafi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati