Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya zoezi katika Halmashauri yake. Ndg. Fwema ameeleza Halmashauri yake imekuwa ikiendesha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa kushirikiana na NIDA vizuri ikiwa ni pamoja na kutoa Ofisi kwa NIDA ya kuendeshea Usajili kwa wananchi.
Aidha Halmashauri yangu kwa kushirikiana na NIDA tumefanikiwa kukamilisha kufanya Usajili wa watumishi wa umma ambapo kwa sasa tunaendelea na Usajili wa Mkupuo (Mass Registration) kwa wananchi na zoezi linaendelea vyema na hatujakwama popote ukiachilia mbali changamoto mbalimbali zinazojitokeza za hapa na pale ambazo kwa mashirikiano ya pamoja tunazikabili na kupata ufumbuzi.
Ndg. Fwema amewataka Wananchi kugawa muda wa kilimo na wa kujiandikisha ili waweze kutumia fursa hii ya Usajili wa Mkupuo unaoendelea kwani ni agizo la serikali na ni la lazima. ''Ni vyema wananchi mkajitokeza kipindi hiki ambacho huduma imesogezwa karibu nanyi ama sivyo itawalazimu kufuata huduma hii katika ofisi ya NIDA pindi watakapokamilisha Usajili wa mkupuo katika Halmashauri ya Mji wa Babati''.
Ametoa pongezi kwa vyombo vya habari katika kutumia vyombo vyao kuelimisha umma na kuwasihi kutochoka kutekeleza jukumu hilo. Akihitimisha mazungumzo yake na waandishi Ndg. Fwema amewataka watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa NIDA hususan katika kuhamasisha umma kwa kutoa taarifa juu ya zoezi linaloendelea na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo ya msingi wanayotakiwa kujiandaa nayo kabla ya kufika katika vituo vya Usajili.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati