• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Ujumbe wa Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021

Imechapishwa: June 14th, 2021

Na Nyeneu, P. R

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Jacob Twange pamoja na viongozi wengine kwa kushirikiana na watumishi na wananchi wilayani humo jana tar 13 mwezi Juni ameupokea Mwenge wa Uhuru Pamoja na wakimbiza mwenge kitaifa na viongozi wengine kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Kanali Patrick Songea. Katika wilaya Babati Mwenge umekimbizwa katika sehemu mbalimbali na kukagua miradi mikuu mitano (5) ambayo ni uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa mabweni ya kisasa katika shule ya sekondari Ayalagaya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya, uzinduzi wa Katiba ya kikundi cha wajasiriamali wa Boda boda, huu ukiwa ni mradi wa Pikipiki unaotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Babati kupitia kitengo cha Maendeleo ya Jamii na Ustawi.

Mradi wa tatu ni mradi wa Maji uliopo katika Kijiji cha Imbilili katika Halmashauri ya Mji. Mradi uliofuata ni Matumizi ya Tehama katika vituo vya kutolea huduma za afya katika Kituo cha Afya cha Magugu kilichopo Halmashauri ya Wilaya na mwisho ilikuwa ni uwekaji wa jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya katika Kijiji cha Mwada pamoja na kuzindua klabu ya wapinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Magugu na baadae Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa amekagua Mabanda mbalimbali likiwemo banda la TEHAMA Wilaya ya Babati. Mhe. Mkuu wa Wilaya pamoja na wananchi ameukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang leo tarehe 15 Juni baada ya mkesha katika Uwanja wa Kwaraa uliopo mjini Babati.

Tukumbuke kuwa, Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyiaka kila mwaka katika maeneo mbalimbali nchini. Mbio hizi huanza na tukio la kuwashwa kwa mwenge katika mkoa uliochaguliwa kitaifa, ambapo mwaka huu mbio maalum za Mwenge wa Uhuru zimezinduliwa rasmi na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdul huko Mkoani Kusini Unguja visiwani Zanzibar kisha kukimbizwa mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani kutoa tumaini, kuhamasisha ushiriki katika miradi ya maendeleo pamoja na kuhamasisha amani.

Mbio hizi huwa na kauli mbiu ambazo huchaguliwa kila mwaka kutokana na vipaumbele vya maendeleo kitaifa ambavyo huendana na uzinduzi wa miradi ya maendeleo katika maeneo unapopita. Mbio hizi maalum za Mwenge mwaka 2021 zinaambatana na ujumbe wa Matumaini, Upendo, Amani na Heshima.

Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Paul Mwambashi amewaeleza wananchi kwamba Mwenge wa uhuru 2021 haujaja bure lakini umekuja na ujumbe mahususi kwa ajili ya kuendelea kuchochea maendeleo ya Taifa letu. Ujumbe mkuu wa mbio za Mwenge mwaka 2021 unahusu matumizi sahihi ya TEHAMA chini ya kaulimbiu isemayo “Tehama ni msingi wa Taifa endelevu, itumie kwa usahihi na Uwajibikaji”. Kupitia kaulimbiu hiyo, Luteni Josephine amesema Teknolojia hii ya Mawasiliano ni nyenzo muhimu na ya kisasa katika kuleta maendeleo kiuchumi, kielimu, kijamii na kiutamadani. Wananchi kwa ujumla tunaendelea kukumbushwa kutumia TEHAMA kwa usahihi na si vinginevyo. “Lakini pia teknolojia hii inaendelea kusisitiza makusanyo ya mapato kwa njia ya kielektroniki”, Alisema Luteni Josephine.

Lakini pia mbio hizi Maalum za Mwenge zinaendelea kusisitiza katika mapambano dhidi ya Rushwa chini ya kaulimbiu isemayo “Kupambana na Rushwa ni jukumu langu”. Rushwa ni adui wa haki, pia Rushwa inarudisha maendeleo nyuma na Serikali kwa kulitambua hilo ilianzisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Vilevile mbio hizi maalum za mwenge wa Uhuru 2021 zinaendelea kusisitiza mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria chini ya kauli mbiu isemayo “Zero Malaria inaanza na mimi, nachukua hatua kuitokomeza”. Ugonjwa wa Malaria umekuwa ni tishio hasa kwa Watoto wadogo na akina mama wajawazito. Wananchi kwa ujumla tunaendelea kusisitizwa kuhakikisha tunachukua tahadhari za kupambana na ugonjwa wa Malaria ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika mazingira tunayoishi, kufukia madimbwi ili kuua mazalia ya Mbu lakini pia kulala kwenye Chandarua chenye dawa.

Sambamba na hayo, mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 zinaendelea kusisitiza mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kwani dawa za kulevya zimekuwa ni tishio hasa kwa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa letu. Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa amewasihi sana wanafunzi kuepuka vishawishi na makundi ambayo yanaweza kuwasababishia kuanza kutumia dawa za kulevya.

Mwisho kabisa mbio maalum za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 zinaendelea kutoa ujumbe wa mapambano dhidi ya virusi vya UKIMWI chini ya kaulimbiu isemayo “Mshikamano wa Kitaifa tuwajibike kwa pamoja”. Ugonjwa wa UKIMWI umeendelea kumaliza vijana na hasa vijana wa Kike kutokana na kuendelea kukithiri kwa biashara ya ngono kwa watoto wa Kike. Lakini pia mbio hizi maalum zinaendelea kusisitiza ulaji wa Lishe bora kwa ajili ya kupata afya imara. “Ndugu wananchi, lishe bora ni msingi wa kumjenga mtoto vizuri kimwili na kiakili” Ameeleza Luteni Mwambashi.

Picha zote na Nyeneu, P. R

Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati