Na Nyeneu, P. R
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amewaagiza wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Biashara kwenye Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya vya mapato na kutenga 10% ya mapato hayo kwaajili ya vikundi vya wajasiriamali ili kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na hata pia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
RC Makongoro ametoa maelekezo hayo kwenye kikao kazi maalum cha kujadili namna ya kuongeza mapato na usimamizi wa mapato hayo katika mwaka mpya wa fedha 2022/2023 ili kuleta tija kwenye uchumi mkoani hapa na kwa taifa. Baadhi ya vikundi vya vijana vinaeleza namna wanavyonufaika na mapato ya Serikali kupitia 4% inayotokana 10 % ya mapato ya ndani kwenye halmashauri.
Katika kikao hiki Mkoa wa Manyara umetoa tuzo na vikombe vya pongezi kwa Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiongozwa na mbulu ikifuatiwa na Simanjiro ambapo Halmashauri ya Mji wa Babati ikishika nafasi ya kumi na saba (17) ikiwa na alama 84.3 Daraja A
Mkoa wa Manyara una Halmashauri Saba (07) ambazo kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa nchi OR-TAMISEMI Innocent Bashungwa mapema wiki iliyopita, Halmashauri Nne (04) ambazo ni Mbulu Mji, Simanjiro, Babati Mji na Hanang ambazo zimeingia 20 bora katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri zote zikiwa na daraja A.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati