Katika Kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima nanenane Kanda ya Kaskazini Viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha Mgeni rasmi MKuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga amesisitiza Ufugaji,Kilimo pamoja na Uvuvi wa kisasa katika jamii ili kuweza kupata tija.
Pia amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha vitendea kazi vya kisasa na wawekezaji ambavyo vimeleta matokea chanja kwa shughuli za Kilimo,Ufugaji na Uvuvi pamoja na kuandaliwa vyema kwa mafunzo kwa Maafisa Ugani ili wawaze kutoa elimu kwa wananchi na kuleta mabadiliko.
Aidha Mhe.Sendiga amesema kuwa elimu ambayo imetolewa katika maonesho hayo na washiriki mbalimbali wananchi wametakiwa kuitumia ili kupata maendeleo katika uchumi na kuwa na kilimo chenye tija pamoja na shughuli nyinginezo katika jamii hii itasaidia pia kukabiliana na changamoto ya utapiamlo katika jamii hivyo mfugaji,mkulima na mvuvi kuhakikisha shughuli zako zinaenda kisasa.
Vilevile ameongeza kuwa Ufugaji wa kisasa utasaidia kupunguza migogoro ambapo kwa sasa idadi ya watu imeongezeka na mifugo hivyo ikitumika njia ya kisasa katika ufugaji inatumia eneo ndogo na migororo itapungua kati ya wakulima na wafugaji.
Mhe.Sendiga amewataka Viongozi washughulikie 20% kwenye ushuru wa mazazo na mgawanyo wa 15%kwenye Mifugo na 5%kwenye Uvuvi umezingatiwa ili kuendeela kupata maboresho na kutumia vitendea kazi vya kisasa.
Sambamba na hilo Mhe.Queen amesema kuwa zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa katika daftari la kudumu limeendelea kwa baadhi ya Mikoa hivyo amewasisitiza wananchi wenye umri husika kujitokeza kwa wingi pindi zoezi hilo litakapoanza na ameongeza kuwa wanawake wajitokeze kwa wingi katika kuwania nafasi za Uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara tu muda wa kuchukua fomu ukitangazwa.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati