Na Nyeneu, P. R
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mhe. Paulina Gekul, Jumamosi ya Agosti 13, 2022 ameongoza zaidi ya wakimbiaji 100 kushiriki Mbio za Manyara International Marathon 2022 zilizofanyika Mjini Babati katika viwanja vya Kwaraa.
Mbio hizo zilizohusisha wadau mbalimbali zimeandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Paulina Gekul na kudhaminiwa na kampuni ya Vinywaji ya Bonite ambao wametoa fulana kwa wahiriki na fulana za mazoezi kwa washindi wote.
Mhe. Mbunge alishiriki mbio za Kilomita 5 na kuwaongoza viongozi kadhaa, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange, Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg. Khalfan Matipula, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Abdulrahman Kololi, Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bi. Anna Fisoo, viongozi wengine wengi kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali.
Vile vile Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara wamejitokeza katika uzinduzi wa Mbio hizo na kushiriki mbio za Mita 100, Kilomita 10 na pia Kilomita 21 na washindi wakapewa zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kwa mshindi wa kwanza, wa pili na watatu na fulana za mazoezi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati