Mhe.Queen Sendiga amefanya jogging iliyopewa jina la Manyara Daftari Day ambayo imeandaliwa kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024Jogging hiyo imeudhuriwa na Viongozi wa Vyama na Serikali pamoja na wananchi .
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Sendiga amesisitiza wananchi ambao wamefikisha umri wa kupiga kura wakajiandikishe mara tu zoezi litakapoanza,waliohama au kupoteza kadi zao kwenda kuboresha taarifa pia kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi.
Aidha Mhe.Sendiga amewashukuru Viongozi wote wa Mkoa wa Manyara pamoja na wananchi kujitokeza kushiriki katika Jogging hiyo maalum katika Mkoa wa Manyara.''Imarisha Afya Yako,Jindikishe na Kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Jamii Endelevu''.
‘’Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora’’.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati