Wadud waharibifu viwavijeshi aina ya "Fall Armyworm" wanaoshambulia majani ya aina mbalimbali ya mimea wamevamia maeneo ya mashamba katika Halmashauri ya Mji wa Babati.Akizungumza kuhusiana na wadudu hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bwana Fortunatus H.Fwema amesema kuwa wadudu hao wanashambulia kwa haraka zaidi zao la mahindi shambani kiasi ambacho wanaweza kumaliza au kuathiri shamba zima ndani ya muda mfupi endapo hawatadhibitiwa kwa wakati.Nae Mkuu wa Idara ya Kilimo, umwagiliaji na ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bwana Daniel Luther alisema VIUADUDU vinavyoshauriwa kutumika ni vile vyenye mchanganyiko wa vimeng'enyo muhususi zaidi ya kimoja kama vile Duduba 450EC,Cyclone, Farmguard,Protrin 60EC,Perfecto 175SC, Blast, Tanzapana 344SE, Tanzatoto 550EC au Tanzachlro.Mkuu huyo wa Idara aliwashauri wakulima kutumia Duduba 450EC,Cyclone, Farmguard, Protrin 60EC ambazo zinapatina kwenye maduka ya pembejeo kwa sasa.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bwana Fwema aliwashauri wakulima wote kuhakikisha wananyunyuzia VIUADUDU ili kudhibiti mzunguko na uzalianaji wa wadudu hao hatari, pia aliwataka wakulima wanapotumia VIUADUDU wafuate maelekezo kutoka kwa Maafisa ugani waliopo kwenye ofisi za kata zote nane za Halmashauri ya Mji Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati