Kamati ya Fedha na Uongozi imetembelea miradi ya maendeleo katika sekta ya Elimu na Afya kwa Kata zote nane ndani ya Halmashauri ya Mji wa Babati ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman H. Kololi, Madiwani ,Wajumbe wa Kamati pamoja na Wataalam Mkoani Manyara.
Lengo la kamati hiyo ni kukagua na kutembelea miradi ambayo imekamilika na inatumika pamoja na ile ambayo ujenzi unaendelea na kupata taarifa kamili za miradi husika na namna fedha za mapato ya ndani na Serikali kuu zimetumika kwa umakini na ufasaha katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024 katika miradi yote ya maendeleo.
Kamati imetembelea madarasa mawili na Ofisi katika Shule ya Msingi Ayabadney ambapo mradi umekamilika na wanafunzi wanendelea kutumia vyumba hivyo vya madarasa changamoto ni matundu ya vyoo vya Walimu,Kamati imemtaka Afisa Mtendaji kuwasilisha changamoto hiyo katika kamati ya maendeleo ya Kata{WDC}.
Vilevile Kamati imetembelea nyumba ya Walimu Shule ya Sekondari Pauline Gekul, Ujenzi bado unaendelea na umefikia hatua ya umaliziaji na Kamati ya Fedha na Uongozi imewataka kamati ya Ujenzi kuhakikisha malipo ya fundi yanafanyika kwa uharaka ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.
Sambamba na hilo kamati imetembelea mradi wa Ujenzi wa Darasa moja Shule ya Msingi Gendi mradi umekamilika,Nyumba wa Walimu Shule ya Msingi Bambay mradi upo hatua ya umaliziaji,Madarasa mawili Shule ya Msingi Ziwani ujenzi umekamilka,Ujenzi wa madarasa mawili ya mfano na matundu sita ya vyoo Shule ya Msingi Hangoni mradi umekamilika,Ukamilishaji wa Zahanati Chemchem pamoja na kichomea taka pamoja na Ujenzi wa darasa moja Shule ya Msingi Chemchem.
Mhe.Kololi amesema kuwa kwa miradi ambayo haijakamilika kwa wakati amewataka Viongozi kuendelea kuwa bega kwa bega na fundi ili mradi ukamilike na kuweza kutumika mara moja. Kamati imetoa ushauri na maoni kwa miradi ambayo ina changamoto.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati