Halmashauri ya Mji wa Babati imetoa mafunzo kwa vikundi 19 vilivyopata mikopo ya 10% kwa ajili ya shughuli za kiuchumi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanufaika hao kusimamia mikopo hiyo kwa ufanisi. Pamoja na matumizi sahihi ya mikopo, kutunza kumbukumbu na kuwahimiza kuwashirikisha Wataalam katika shughuli zao za kiuchumi ili mikopo hiyo iweze kuwa na tija kwa Jamii.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw.Ally Mwinyikombo ameeleza kuwa vikundi nufaika kwa awamu ya kwanza ni vikundi vinavyojihusisha na shughuli za Usafirishaji,Ufugaji,Kilimo na Biashara. Pia ameongeza kuwa mpango huo unalenga kuwasaidia wanufaika kujiajiri, kuongeza kipato cha familia zao, na kuchochea Maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika Mji wa Babati.
Aidha katika mafunzo hayo Afisa usalama Barabarani Koplo Dotto Aloyce amewataka madereva wa Bodaboda kukata Bima ya vyombo vya moto na amewahimiza kuzingatia Sheria za usalama Barabarani wanapofanya shughuli zao za usafirishaji.Pia ameongeza kuwa usalama ni muhimu kwao na kwa jamii nzima, hivyo ni vyema kuwa makini Barabarani ili kuepusha ajali na madhara mengine.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati