Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Kitila Mkumbo amezindua rasmi Kituo cha Afya cha Sigino Pamoja na jengo la wodi ya Watoto lililofanyiwa ukarabati Hospitali ya Mji Babati(Mrara) Halmashauri ya Mji wa Babati.
Ujenzi wa Kituo cha Afya umegharimu takribani Millioni 430, Millioni 30 zikiwa ni pesa kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri na Millioni 400 ni pesa kutoka Serikali Kuu, ukarabati wa jengo la Watoto umegharimu Millioni 25 pesa kutoka Serikali Kuu.
Mhe. Mkumbo ameeleza kuwa mpango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za Afya maeneo ya karibu, kwa kuwa uwepo wa huduma za afya maeneo ya karibu utasaidia wananchi kupata huduma kwa haraka na kupunguza vifo vya mama wajawazito na Watoto.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Pauline Gekul amemshukuru Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu kwa kutoa pesa kwa ajili ya miradi hiyo pia ameeleza kuwa kituo cha Afya bado kinakabiliwa na changamoto ya huduma ya upasuaji.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati