Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Mhagama ametembelea Kituo cha Hali ya Hewa kinachojiendesha chenyewe ( Automatic Weather Station) kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Babati na kuwataka wananchi wa Babati kukitumia kituo hicho vizuri ili kiweze kuwaletea maendeleo kwani kwa kufuatilia utabiri unaotolewa na kituo hicho wananchi wa Babati watapata uhakika wa kujua hali ya hewa katika Mji na itawasaidia sana wakulima,wafugaji, wakandarasi,watafiti na wanafunzi.
Akisoma risala kwa Mheshimiwa waziri Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki Bi.Juwairia K. Mshana alisema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa ni kuhakikisha takwimu zinasaidia usalama wa wananchi na mali zao kwa kutoa tahadhari kwa matukio kama upepo mkali, Mvua kubwa na Mafuriko ambayo yanaweza kuwakumba wananchi na mali zao kwa kutoa tahadhari.
Kituo hicho cha hali ya hewa kimejumuisha Kipima Mvua, (Automatic rain gauge), Kipima Upepo ( Wind van and anemometer) Na Kipima Mgandamizo wa hali ya Hewa (Barometer).
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wa Babati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Babati Bwana Fortunatus H. Fwema alimuhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa watashirikiana na wataalamu wa Hali ya Hewa waliopo kituoni hapo ili kuhakikisha kituo hicho kinaleta manufaa kwa wananchi wa Babati na maeneo jirani pamoja na kukitunza kwani wanafahamu gharama za kujengwa kituo kicho.
Kituo hicho ni moja kati ya vituo 36 vilivyopo Tanzania nzima na kwa upande wa Nyanda za juu kaskazini vipo vituo sita tu.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati