Na Nyeneu, P. R
Halmashauri ya Mji wa Babati kupitia Hospitali ya Mji, leo tarehe 17 Mei 2021 imefanya uzinduzi wa mpango wa usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Katika mpango huo, Halmashauri imejipanga kusajili na kutoa vyeti kwa watoto wapatao elfu kumi na sita mia Saba sitini na nne (16,764) ikiwa ni bila malipo. Aidha Katibu Tawala Wilaya ya Babati Ndg. Halfani Matipula akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Mkuu wa Wilaya Mhe. Lazaro Twange, ameishukuru sana Serikali kupitia RITA kwa kuleta mpango huo wa vyeti bure katika katika Mkao wa Manyara na wilaya zake zote.
"Kipekee niishukuru Serikali kwa kuupokea mpango huu na kupitia RITA kuona kwamba kati ya mikao ambayo watapeleka programu hii ni pamoja na Mkoa wetu wa Manyara na kipekee kwa Wilaya yetu ya Babati kwa Halmashauri zote mbili". Alisema DAS.
Uzinduzi wa mpango huu umekuwa ni mwendelezo ambapo wiki iliyopita ulifanyika Halmashauri ya Wilaya ulifanyika katika Kijiji cha Magugu. Ndg. Matipula ameeleza kuwa ili kufikia malengo tuliyojiwekea katika uandikishaji ni lazima taarifa zipelekwe kwa watu wote huko majumbani, hii ni kwa sababu watoto ambao wanapaswa kunufaika na huu mpango si wale tu ambao wazazi wao washiriki katika zoezi la uzinduzi.
Watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wanapaswa kuandikishwa na kupatiwa vyeti, na akina mama wasiogope kuwaandikisha watoto wao bila kujali idadi ya watoto alionao.
Sambamba na hayo, pia DAS amesisitiza uadilifu kwa wale watoa huduma wawe mstari wa mbele kuwaambia wananchi kuwa cheti kinatolewa bila malipo yaani bure. Kwani kufanya kinyime na mpango hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yule ambaye atakiuka utaratibu huo wa uandikishaji na utoaji wa cheti bure.
"Nawaomba sana wale ambao wamepewa majukumu haya wasije hata mara moja wakashawishika kuwaambia wananchi kwamba au kuchukua fedha kwaajili ya kutoa cheti". Amesisitiza Mgeni rasmi. Vile vile Mhe. Mgeni rasmi amewaonya wazazi kutokuthubutu kuwasajili watoto amba sio rai wa Tanzania na wala wasihusike katika kutoa taarifa zao kwa sababu mipango hii ni ya Tanzania na ni kwaajili ya watanzania.
Aidha, Afya Afya Halmashauri ya Mji Bw. Aretas Leurent akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mji katika Hotuba yake ameeleza malengo yao kama Halmashauri katika kuhakikisha zoezi la uandikishaji na utoaji wa vyeti linafikia malengo na pia ameeleza faida za cheti cha kuzaliwa kwa mtu mmoja mmoja.
Aidha, Afisa Kutoka RITA Mkoa wa Manyara na ni Mratibu Msaidizi wa Zoezi hili la uandikishaji na utoaji wa vyeti bure kwa watoto chini ya miaka mitano Ndg. Temba ameeleza kuwa vyeti hivyo si bure kwa maana ya kuvifanya vikakosa thamani. Akaendelea kwa kusema kwamba vyeti hivyo vimegharamiwa na Shirika la UNICEF ambapo cheti kimelipiwa sawa na vyeti vingine.
Gharama iliyotumika kukigharamia cheti hiki ni sawa na gharama ya vyeti vingine. Mpango huu uwe ni fursa kwa Wananchi wa Mkoa wa Manyara hususani Wilaya ya Babati na Halmashauri zake zote. Kabla ya mpango, gharama ya kupata cheti cha kuzaliwa ilikuwa ni kubwa kwa maana ya usafiri na muda ukilinganisha na sasa ambapo mtoto wa miaka chini ya mitano atakipata bure na huduma itamfikia popote pale alipo.
Bw. Temba ametoa rai kwa wananchi kuvithamini vyeti hivyo vinavyotolewa sasa kama wanavyovithamini vile vingine vinavyotolewa maofisini kwani cheti hicho ni sawa na kile ambacho kinapatikana Ofisi za RITA. Cheti hiki kipewe matunzo sawa na kile cheti ambacho umekilipia, Matumizi ni yake yale yale ambayo yangetumika na cheti kile ambacho ungekichukua ofisi za RITA.
Picha zote: Nyeneu, P. R
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati