Na Nyeneu, P. R
Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokea kwenye shingo ya kizazi cha mwanamke - ambayo ni kiingilio kutoka uke hadi katika mfuko wa uzazi.
Ni moja kati ya zaidi ya aina 100 ya virusi vya human papilloma (HPV), ambavyo 13 vinasababisha saratani. Pia aina fulani ya HPV vinaambukizwa kwa njia ya ngono.
Baadhi ya sababu za kupata ugonjwa huo ni kushiriki ngono ukiwa na umri mdogo, ukifanya ngono na washiriki wengi , kuvuta sigara na kuwa na virusi vya Ukimwi.
Dalili ni
Uchunguzi wa virusi hivyo unastahili kufanyika ili kuvigundua mapema. Chanjo za HPV ni hatua nyingine ya kuziuzi.
Matibabu kwa wagonjwa walio na virusi hivyo yanategemea na viwango vya virusi hivyo mwilini, hata hivyo yanaweza hitaji kutibiwa kwa njia ya upasuaji na kutoa sehemu au mfuko wa uzazi mzima au kutumia miyonzi.
Chanzo: Shirika la Afya duniani
Aidha, Halmashauri ya Mji wa Babati kupitia Idara ya Afya kitengo cha Afya Kinga (Chanjo) inaendelea kutekeleza maagizo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wototo kuhusu utoaji wa chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka kumi na Nne (14) na chanjo hii hutolewa kila mwaka. Wasichana wote waliofikia umri wa Miaka 14 huchanjwa chanjo mara mbili, dozi ya kwanza hutolewa anapofikia umri wa miaka 14 na dozi ya pili hutolewa kwa msichana baada ya miezi sita toka dozi ya kwanza. Zoezi hili linaongozwa na Idara ya Afya chini ya John Faustine (Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji Babati) na Beatrice Mlay (Mratibu Msaidizi wa chanjo)
Mratibu wa Chanjo Halmashauri wa Mji wa Babati Bw. John Faustine alieza ukweli wa chanjo hii ambayo watu wengi wamekuwa wakiitafsiri kwa Namna tofauti tofauti.
Ukweli kuhusu Saratani ya Mlango wa Kizazi:-
Chanzo: Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wototo.
Hadi kufikia Tarehe 24 Mwezi April 2021 Timu imefanikiwa kuchanja wanafunzi 620 kati ya walengwa 1572 katika shule 31 kati ya shule 52 zilizopo Halmashauri ya Mji.
Picha zote na Nyeneu, P. R
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati