• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa Taka Ngumu
    • Ofisi ya Mtendaji wa Kata
    • Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa/Kijiji
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Biashara
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
    • Utoaji wa Vibali vya Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Uhakiki wa Kaya za Walengwa wa kipindi cha Pili cha awamu tatu ya TASAF

Imechapishwa: July 13th, 2020

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar inafanya uhakiki wa walengwa wa TASAF ili kupata orodha halisi ya walengwa wa kipindi cha Pili cha awamu ya Tatu ya TASAF wanaokidhi vigezo. Uhakiki wa walengwa utafanyika katika Vijiji, Mitaa na Shehia zote.

Katika semina fupi ya mafunzo ya namna ya kutumia njia ya Kielektroniki kuhakiki taarifa za walengwa, iliyofanyika Katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati tarehe 13 hadi 14 Julai 2020, Muwezeshaji kutoka TASAF makao makuu, Bwana Donald Mziray alieleza madhumuni ya mpango katika kipindi cha Pili cha awamu ya Tatu ya TASAF kuwa mpango umelenga Kuziwezesha kaya za walengwa kutumia fursa za kuongeza kipato na huduma za jamii na uchumi na kuwekeza katika kuendeleza watoto wao. 

Semina hiyo fupi iliwashirikisha wakuu wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mratibu wa TASAF Halmashauri, na wawezeshaji wa mpango. Katika ufunguzi wa semina hiyo, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Ndg. Daniel Luther kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mji alimpongeza Mratibu wa TASAF Halmashauri Bi. Edna Moshi kwa usimamizi mzuri kipindi cha utekelezaji wa Mpango kwa awamu ya kwanza.

Muwezeshaji kutoka TASAF makao makuu aliendelea kuwaeleza wanasemina kuwa katika kipindi hiki cha pili, mpango unasisitiza yafuatayo: -



  • Kuwezesha kaya kufanya kazi na hivyo kuongeza kipato,

  • Kuwezesha kaya za walengwa kuongeza rasilimali zalishi na kuongeza vitega uchumi,

  • Kuwekeza katika rasilimali watu hususan watoto ili kuleta matokeo chanya yatakayodumu kwa muda mrefu,

  • Kuboresha upatikanaji wa huduma za maji, afya na elimu,

  • Kukuza uchumi wa eneo unakofanyika utekelezaji kutokana na matokeo ya Mpango.

Sehemu Kuu za Mpango

1. kujihusisha na programu za jamii

2. Kuimarisha Taasisi na Mifumo

Kufanya tathmini ya Mpango, Kuendelea na muundo wa sasa wa utekelezaji, Kuhitimu kutoka kwenye Mpango - kuweka mfumo wa kutambua kaya zilizopiga hatua kutoka kwenye umaskini, Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji na kuimarisha Masjala ya Kaya za Walengwa. 

Ushiriki wa walengwa – Kujenga uelewa wa walengwa kuhusu stahili zao, kuimarisha mfumo wa kushughulikia malalamiko na mifumo ya kuimarisha uwajibikaji.

Malipo ya ujira – Kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki nchi nzima.

Kujenga uwezo – Kuimarisha mikutano ya kujenga uelewa wa walengwa, kujenga uwezo wa Kamati za Usimamizi za Jamii na Watumishi wa Ugani. Pia, Kufanya uhamasishaji kuhusu masuala ya lishe, uzazi salama na kuimarisha shughuli za kiuchumi, Kujenga uwezo wa Kamati za Usimamizi za Jamii kuhusu manunuzi ngazi ya Jamii na Sera za Kulinda Watu na Mazingira, Kufanya mapitio ya mfumo wa motisha kwa Kamati za Usimamzi za Jamii na Watumishi wa Ugani.

Ndani ya kipindi cha utekelezaji kilichofanyika kati ya mwaka 2013 hadi 2019, baadhi ya kaya za walengwa zimepoteza vigezo na hivyo zinatakiwa kuondolewa kwenye Mpango. Kaya hizi ni za mlengwa ambaye:

  1. Amefariki na hakuwa na wategemezi/ mtegemezi.

  2. Amehamia eneo ambalo Mpango haujaanza kutekelezwa.

  3. Hakufika kupokea malipo mara mbili mfululizo.

  4. Amepata nafasi ya uongozi katika ngazi ya Kijiji/ Mtaa /Shehia.

  5. Ni mjumbe wa Kamati ya jamii ya usimamizi wa Mpango (CMC).

  6. Mwajiriwa anayepokea mshahara.

  7. Aliingia kwenye Mpango na hakuwa maskini.

Bwana Donald (Muwezeshaji) aliendelea kuwaeleza wanasemina wote kuwa kaya za walengwa ambao waliingia kwenye Mpango wakiwa na hali duni na sasa hali zao zimeimarika kiuchumi nazo zitahakikiwa na baadae utaratibu maalum wa kuziondoa kwenye Mpango utafuata. 

Aidha utaratibu utakaotumika kuhakiki walengwa ni kutumia njia ya ukaguzi wa vitambulisho vya mlengwa na baadae yatafanyika mahojiano ya ana kwa ana na mwakilishi wa kaya ili kukusanya taarifa kwa njia ya dodoso fupi na kuhuisha taarifa zote za wanakaya ikiwemo umri, darasa (kwa wanaosoma), mahudhurio ya kliniki katika kituo cha huduma za afya (kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano), wenye uwezo wa kufanya kazi, wanakaya wapya, wanakaya waliofariki, wanakaya waliohama na wanakaya wenye ulemavu.

Sambamba na hilo, kaya za walengwa ambao wameimarika kiuchumi zinaweza kujiondoa kwenye mpango kwa hiari kwa kuandikisha majina yao kwa Viongozi wao wa Vijiji/Mtaa/Shehia. kupitia zoezi la uhakiki wa taarifa zitakazopatikana kwa njia ya kujaziwa dodoso, kaya itakayokosa vigezo kwa kuimarika kiuchumi itaondolewa kwenye Mpango hata kama kaya hiyo haikuorodhesha jina kwa kiongozi wa sehemu husika ili iondolewe kwenye mpango.


Imeandikwa na Nyeneu, P. R



Matangazo

  • TERMS OF REFERENCE FOR CONSTRUCTION SUPERVISION CONSUTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BABATI TOWN UNDER TACTIC PRJECT TIER 2 March 07, 2025
  • Tangazo la kuitwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili 2025. May 08, 2025
  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Timu ya Menejimenti Halmashauri ya Mji Babati imefanya Ziara kukagua Miradi ya Maendeleo

    May 07, 2025
  • Watumishi Manyara wametakiwa kupendana na kuacha chuki.

    April 30, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amewataka Wananchi kuuenzi Muungano.

    April 26, 2025
  • Chanjo nyongeza ya polio (IPV2) kuanza kutolewa kwa watoto wa miezi 9 mwezi wa tano 2025.

    April 24, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Makala ya Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Babati 2024
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati