Na.Evaline Komba
Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Halmashauri ya Mji wa Babati Bw. Simon Mumbee akishirikiana na Maafisa Taaluma wa Divisheni hiyo, leo tarehe 4 Agosti, 2023 amefanya kikao maalum na Wakuu wa Shule katika Ukumbi wa Mji kujadili maswala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa KPI.
Katika kikao hicho, Wakuu wa Shule na Maafisa Elimu wamesisitizwa usafi wa mazingira kwa kupanda miti na kuwahimiza wanafunzi kuendelea kufanya usafi wa vyoo ili kuepukana na maradhi hasa yale ya mlipuko, hivyo wametakiwa kuvitunza sana.
Pia walimu wamekumbushwa kushirikiana na Wazazi kujua idadi kamili ya Wanafunzi waliotoa na ambao hawajatoa chakula shuleni , wanafunzi wote wanatakiwa kupewa chakula wanapokuwa shuleni na kipindi wanapofanya mitihani .
Walimu na Wazazi kwa pamoja wametakiwa kuhakikisha kila mzazi anatoa chakula kwa wakati shuleni ili wanafunzi wote wapate chakula muda wa kula kwa kufanya hivyo kutasaidia pia ufaulu kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Aidha walimu wametakiwa kuwa makini wakati wanaposhughulikia uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine na wakati wa mitihani wametakiwa kuhakiki kwa ufasaha majina ya mwanafunzi na namba yake.
Walimu wametakiwa kuendelea kujituma kufundisha kwa weledi na kuongeza mbinu mbalimbali zitakazosaidia ufaulu kwa wanafunzi kuongezeka.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati