Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji wa Babati CPA.Shaaban A.Mpendu amefungua rasmi mafunzo kwa Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Babati day ambapo mafunzo hayo yameudhuriwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi,Afisa Uchaguzi pamoja na Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga kura.
Wasimamizi wa Vituo vya Kupiga kura wamepewa mafunzo kuhusu dhana ya uchaguzi,kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na namna ya kusimamia mchakato wa zoezi la upigaji kura wanapokuwa katika Vituo vya kupigia kura takribani Wasimamizi wa Vituo vya kupiga kura 220 wamepatiwa mafunzo hayo.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban Mpendu amesisitiza kuwa Uchaguzi umetakiwa kuwa wa huru na haki kwa kufuata maelekezo ya Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika Vituo na kuzingatia mafunzo hayo.
Aidha CPA. Mpendu amesisitiza usiri,uadilifu katika kusimamia zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na matumizi ya lugha inayofaa wakati wa zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika mnamo Tarehe 27/11/2024 na Halmashauri ya Mji wa Babati ina jumla ya Vituo 103 na amesisitiza muda wa kufunguliwa Vituo kuzingatiwa kuanzia Saa 2:00 Asubuhi vituo vinatakiwa kufunguliwa na Saa 10:00 Jioni kufungwa.
Aidha ameongeza kuwa Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi wametakiwa kusimamia zoezi kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na utaratibu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa amewatoa hofu kuwa ulinzi umeimarishwa wakati wote wa zoezi.
Pia Mkufunzi wa mafunzo hayo Bi.Edna Moshi ambaye ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa amesisitiza umakini,uaminifu na uadilifu katika zoezi la Uchaguzi ili wananchi waweze kupata Viongozi kwa haki na kwaajili ya maendeleo ya wananchi wa eneo husika.
Sambamba na hilo Wasimamizi wa Vituo vya kupiga kura wametoa kiapo cha utii mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Bw.Jumaa.M.Mwambago na wamesisitizwa kuzingatia Sheria,Taratibu na Kanuni za Uchaguzi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati