Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Babati Bw.Gasto Silayo amewataka Wananchi kuendelea kuhamasishana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la Mkazi ili waweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Bw.Silayo amesisitiza kuwa ili uweze kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lazima ujiandikishe amesema hayo alipokuwa katika Mkutano na Wananchi wa Kitongoji cha Chemchem Kata ya Mutuka Halmashauri ya Mji Babati.
Wananchi wa Kitongoji Cha Chemchem ambao tayari wamejiandikisha wameazimia kushirikiana na mabalozi wao kuwahamasisha Wananchi wenzao ambao bado hawajajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kujiandikisha kwa siku ambazo zimesalia.
Sambamba na hayo zikiwa zimesalia siku tatu Wananchi wa maeneo tofauti tofauti katika Halmashauri ya Mji wa Babati wameendelea kujiandikisha kwenye daftari la wakazi katika vituo vyao.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati