Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emmanuella Mtatifikolo Kaganda ametumia usafiri wa pikipiki ya matairi matatu maarufu kama bajaji ili kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Babati kujitokeza kushiriki kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Mhe. Kaganda ametumia usafiri huo kuzunguka maeneo kadhaa ya Mji wa Babati ikiwa pamoja na kwenye vituo vya maafisa wasafirishaji(bodaboda)na maeneo ya wajasiriamali wadogo kama mama lishe na wafanyabiashara wengine.
Pia Mhe Emmanuella amezungumza na Wananchi kwa kutoa elimu kuhusu uandikishaji wa daftari la mkazi na ule uandikishaji wa kuboresha taarifa zao utakaowasaidia kufanya Uchaguzi Mkuu wa Mwakani 2025.
Aidha Mkuu wa Wilaya Mhe.Kaganda amejiandikisha katika daftari la mkazi katika Kituo cha Mtaa Mrara ambapo na Maafisa usafirishaji takribani 09 ambao ni majirani zake nao wamejiandikisha pamoja nae.
Sambamba na zoezi hilo baadhi ya Maafisa usafirishaji wametoa pongezi zao kwa Mhe. Emmanuella kwa kuweza kushirikiana nao na wamesema kuwa baada ya kujiandikisha wataendelea kufanya hamasa kwa wenzao kwenye Mitaa yao ili wajiandikishe katika Daftari la Mkazi waweze kupiga kura ifikapo Novemba 27,2024.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati