Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi Pendo Mangali amegawa mipira ya miguu kwa Shule ambazo zipo katika mradi wa Football For Schools [F4S] kwa awamu ya kwanza Shule za Msingi takribani tatu zimepata mipira 40 kwa kila Shule.Katika zoezi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ameongozana na Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bw.Simon Mumbee pamoja na Afisa Michezo,Utamaduni na Sanaa Bw.Jumaa Kifula katika Shule ya Msingi Babati,Maisaka na Kwaang’w katika Halmashauri ya Mji wa Babati.
Afisa Michezo,Utamaduni na Sanaa amesema kuwa Program ya Football for School [F4S] imeanza kwa Shule za Msingi ili kuibua vipaji kwa vijana wadogo wa kike na kiume na kurahisisha ufundishaji wa michezo kwa vitendo Shuleni.Pia ameongeza kuwa Walimu wa michezo kushiriki katika program ya FIFA na TFF kwa kupewa mafunzo mbalimbali.
Aidha ameeleza kuwa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania [TFF] watatoa mafunzo kwa Walimu wa michezo kusimamia program na kuzitembelea Shule za mradi ili kuweza kukagua maendeleo ya mradi pamoja na kuendelea kutoa vifaa vya michezo kwa shule kwa kushirikiana na FIFA.
Bi.Pendo Mangali amewataka Wanafunzi kutumia vizuri mipira hiyo pamoja na kuibua vipaji kwa Wanafunzi hao kupitia vifaa hivyo vya mipira ya miguu katika Shule za Msingi ili kuweza kupata wachezaji wakubwa katika ngazi ya Wilaya,Mkoa na baadae Taifa kwa ujumla.
Sambamba na hilo Wanafunzi wa Shule hizo wameishukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuibua vipaji Shuleni kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya michezo Shuleni.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati