Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. LazaroTwange ametembelea kiwanda cha Dutchkona kilichopo katika eneo la viwanda wa SIDO kinachotengeneza vinywaji vya pombe kali Best na Jogoo na katika ziara hiyo ameambatana na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji wa Babati ikiwemo Mhe.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji,Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya,Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji pamoja na wataalam Mkoani Manyara.
Mhe.Twange amempongeza mwekezaji wa kiwanda hicho kwa kutoa fursa ya ajira kwa vijana takribani 100 ambao wanafanyakazi katika kampuni hiyo, ambayo kwa sasa ipo katika viwanda vidogo vidogo vya wajasiriamali vinavyojulikana kama {SIDO }amewataka vijana hao kuwa waaminifu, kuacha tabia ambazo sio nzuri na kujali muda wa kazi wakati wote.
Vilevile amesema kuwa wapo tayari kushughulikia changamoto zozote zinazowakabili katika uendeshaji wa kiwanda pamoja na wao kuzingatia taratibu na miongozo ya uwekezaji na maelekezo wanayopewa juu ya uendeshaji wa kiwanda katika eneo husika kwa ujumla.Sambamba na hilo amewapongeza kupata eneo jipya ili kuweza kupanua kiwanda ni ishara nzuri ya biashara kukua.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Bi.Pendo Mangali amewataka kuboresha upakiaji wa vinywaji vyao wanavyozalisha, amewapongeza wawekezaji wote pamoja na waliopo ndani ya Halmashauri ya Mji.Halmashauri ya Mji wa Babati ipo tayari kushirikiana bega kwa bega na wawekezaji ili kuhakikisha sekta ya Uwekezaji na biashara imekuwa.
Pia Bw. Norbert John Meneja wa Kampuni ya Dutchkona amesema kuwa biashara ina ushindani mkubwa sana hivyo wamejitahidi kuwatumia maafisa masoko ili kukabiliana na ushindani na matarajio yao ni kutoa fursa ya ajira kwa vijana wengi zaidi wanakapokamilisha ujenzi wa kiwanda chao na amewaomba Viongozi kutembelea eneo ambapo ujenzi unaendelea ili kupata maoni na ushauri kabla ujenzi huo haujafika hatua kubwa zaidi.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati