Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga ametembelea baadhi ya Vituo vya Uandikishaji wapiga kura katika daftari la Mkazi katika Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo ina jumla ya Vituo takribani 90.
Mhe Sendiga ameongozana na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashuari ya Mji wa Babati,Kaimu Katibu Tawala Mkoa,Katibu Tawala Wilaya ya Babati pamoja na Viongozi wengine.
Aidha Mhe.Queen ametoa wito kwa Wananchi ambao wameshajiandikisha kutoa elimu kuanzia ngazi ya kaya ili kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura mkazi katika maeneo wanayoishi.
Pia Mhe.Sendiga amewataka wafanyabiashara wa Soko la Babati,Soko la Silent Innna Wafanyabiashara wa Stendi ya Mkoa wa Manyara kutenga muda kwenda kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kutumia haki yao ya Kikatiba kuchagua Kiongozi wanaomtaka.
Aidha ametoa ufafanuzi kuwa uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la mkazi ni maalum kwa ajili Uchaguzi wa Wenyeviti wa Mtaa,Vijiji na Vitongoji.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati