Mwenyekiti wa Halmashauri wa Mji wa Babati Mhe. Abdulrahman Kololi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika, yaliyoadhimishwa katika kata ya Singe kijiji cha Managha amewataka wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele katika kutokomeza vitendo vya ukatili kama vile ubakaji, ndoa za utotoni, ukeketaji, ulawiti kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo kwani ni jukumu letu kuwalinda watoto.
Aidha, Mhe. Mwenyekiti ameongeza kuwa wazazi kupitia Maigizo na Ngonjera walizoonesha wanafunzi hao leo iwe chachu kwetu kuwa makini na matumizi ya simu zetu kwa watoto kwani yanachangia kwa kasi kubwa kuchochea Mmomonyoko wa maadili.
Pia Bw. Augustino Balao mwakilishi kutoka shirika la COSITA amesisitiza kuwa tutenge muda kwa ajili ya watoto ili tuweze kugundua na kuvikuza vipaji walivyonavyo. Vilevile ameongeza kuwa vitu vinavyomfanya mtoto kuwa imara ni lishe, Afya, Elimu, Malezi, Ulinzi na Usalama katika maisha yao ya kila siku.
Aidha Ofisi ya Mkurugenzi kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii , inaendelea kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia kupitia dawati la jinsia pamoja na kutembelea shule na kutoa elimu. Vilevile Mkuu wa Idara hiyo Bi. Diana Mchonga amewasisistiza wazazi kuwa jukumu la malezi ni la watu wote.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati