Katika kuadhimisha kilele cha wiki ya Mashujaa ambapo kila tarehe 25/07/ ya kila Mwaka tunaadhimisha siku ya mashujaa Duniani.Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara imeadhimisha kwa kufanya usafi katika maeneo ya wafanyabiashara wadogowadogo [machinga].Ambapo zoezi hilo limeongozwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bw.Dominic Mbwette,Watumishi,Wananchi,Viongozi pamoja na Polisi Wilaya ya Babati.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa amewapongeza wote waliojitokeza katika zoezi hilo hakika inapendeza kuwaenzi Mashujaa kwa kufanya jambo ambalo linabaki kuwa kumbukumbu kwetu sote na imekuwa mfano kwa wananchi pamoja na wadau wengine kujifunza kupitia zoezi hilo.
Aidha ameongeza kuwa ni muhimu Mji kuwa safi muda wote na inapendeza kunapokuwa na ushirikiano katika kufanya zoezi hilo.Na amewataka wafanyabiashara kufanya usafi muda wote maeneo yao ya kazi ili kuweka mazingira yanakuwa safi.
Babati bila uchafu inawezekana.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati