Baraza la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Babati limekutana kujadili hoja mbalimbali za Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ukumbi wa Mji leo tarehe 14/06/2023. Baraza hilo limeongozwa na Mh. Queen C. Sendiga Mkuu wa Mkoa Manyara pamoja na Mh. Abdulrahman H. Kololi Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mh.Mkuu wa Mkoa katika mkutano huo alisisitiza kuwa Ofisi ya mkaguzi wa ndani ifanye kazi kwa weledi na kuzingatia sheria ,taratibu na miongozo iliyopo na kuwataka wakuu wa idara wote kudhibiti hoja zisiwepo kwenye vitengo vyao kwani hii itasaidia kutokuwepo kwa hati ya Mashaka.
Aidha Mhe. RC ameongeza kuwa Halmashauri ijitahidi katika kukusanya mapato na kuwataka waliochangia katika kupata hati ya mashaka kuchukuliwa hatua na taarifa zao ziwepo. Pia amesisitiza kuwa kila fedha zinazotolewa zielekezwe kwenye mradi husika na sio kuzihamisha kwenda kwenye miradi mingine.
Kwa upande mwingine Mh. Charles E. Kichele Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amesema kuwa ushirikiano ni muhimu katika Halmashauri ili kukuza na kuendeleza miradi mbalimbali inayosimamiwa na Halmashauri husika.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati